Idadi ya vifo yafikia 2,000 vilivyosababishwa na Tetemeko Nchini Myanmar

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 days ago
rickmedia: idadi-vifo-yafikia-2000-vilivyosababishwa-tetemeko-nchini-myanmar-533-rickmedia

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko la Ardhi lililotokea huko nchini Myanmar inatajwa kuwa zaidi ya watu 2,000 mpaka kufikia leo March 31,2025

Kituo cha Runinga cha Taifa la Myanmar kimeripoti kuwa zaidi ya watu 270 hawajulikani walipo, majeruhi 3,900 na vifo vikiwa 2,056.

Myanmar ilikumbwa na tetemeko la Ardhi Ijumaa ya wiki hii March 28,2025 na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.