ACT"Rais Mwinyi aunde tume huru kuchunguza matukio ya mauaji ya Raia

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 weeks ago
rickmedia: actrais-mwinyi-aunde-tume-huru-kuchunguza-matukio-mauaji-raia-931-rickmedia

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kinalaani vikali tukio la mauaji ya Kinyama dhidi ya Juma Ame Ngwali (58), Mkazi wa Kijiji cha Ndooni, Shehia ya Uweleni, Mkoa wa Kusini Pemba kilichotokea Machi 8, 2025 baada ya kushambuliwa na kikosi maalum kilicho chini ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar (ZDCEA), kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.

ACT imeeleza, mashuhuda wamedai marehemu alipigwa maeneo ya shingo, kuchomwa moto na kukatwa maeneo ya mgongo, kukatwa maeneo ya mikono kwa vitu vyenye ncha kali, ambapo waliotekeleza tukio hilo waliripotiwa kuwa na silaha za moto

Msemaji wa Ofisi, Kamati ya Wasemaji wa Kisekta - Zanzibar, Hamad Mussa Yussuf amesema “Hivyo, inadhihirisha wazi kabisa, matumizi mabaya ya nguvu dhidi ya raia wasio na hatia. ACT tunaamini matendo yote haya yana baraka za Watawala, hakuna Ufuatiliaji wowote unaofanywa na dola, wala hatua walizozichukua, pamoja na raia wema kutoa taarifa na kuonesha mashirikiano ya kina.”

-