Tukio la kusikitisha limetokea katika Uwanja wa Kuykendall, ambapo Austin Metcalf, (kulia) mwanafunzi wa miaka 17, aliuawa kwa kuchomwa kisu na mwanafunzi mwenzake Karmelo Anthony (17) (kushoto) wakati wa mashindano ya riadha ya shule za sekondari.
Kwa mujibu wa ripoti za polisi, ugomvi kati ya vijana hao ulianza kutokana na mzozo wa viti, na hatimaye ukazua mapigano. Austin alifariki akiwa mikononi mwa pacha wake Hunter Metcalf.
Karmelo Anthony amekamatwa na anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya daraja la kwanza. Polisi wa Frisco wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo kamili cha tukio hili la kusikitisha.
Jamii na wanafunzi wa shule husika wametoa rambirambi zao kwa familia ya Austin, huku ibada ya kumbukumbu ikipangwa kufanyika tarehe 9 Aprili katika kanisa la Hope Fellowship.