Shambulizi la Russia laua wanne Ukrain, 14 wajeruhiwa

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: shambulizi-russia-laua-wanne-ukrain-wajeruhiwa-969-rickmedia

Jeshi la Russia limetekeleza mashambulizi ya anga kwa kutumia ndege zisizo na rubani (droni) na kombola la ‘balistiki’ katika Mji wa Kryvyri nchini Ukraine na kusababisha vifo vya watu wanne, huku 14 wakijeruhiwa.

Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa mashambulizi hayo ya Russia nchini Ukraine yametekelezwa usiku kucha wa kuamkia leo Alhamisi Aprili 3,2025.

Mbali na kusababisha vifo na majeruhi mashambulizi hayo yamesababisha uharibifu wa miundombinu nchini Ukraine.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Utawala wa kijeshi wa Mkoa wa Dnipropetrovsk, nchini Ukraine, Serhiy Lysak imesema mashambulizi hayo yalianza jana saa 11:20 jioni ambapo shambulio moja lililenga moja ya viwanda vya jiji hilo.

“Tunaendelea kuthibitisha taarifa. hatari bado ipo. Tafadhali baki mahali salama hadi tahadhari ya mashambulizi ya angani itakapomalizika,” imeeleza taarifa ya Lysak.

Dakika chache baadaye, alitangaza kuwa kwa mujibu wa taarifa za awali, watu wanne walikufa kutokana na shambulio la Russia katika eneo la Kryvyi Rih, huku wengine watatu wakijeruhiwa.