Watu watatu, akiwemo mtoto mdogo, wanaosadikiwa kuwa ni wa familia moja, wamepoteza maisha baada ya kugongwa na gari katika barabara ya Mganza – Chato, eneo la Nyabilele, Kata ya Mganza, wilayani Chato, Mkoa wa Geita.
Watu hao, waliokuwa wakitembea kwa miguu, ni mwanaume pamoja na mwanamke aliyekuwa amebeba mtoto mgongoni.
Hata hivyo, majina yao bado hayajatambuliwa, ingawa inadaiwa kuwa ni wa familia moja waliohamia katika eneo hilo siku za karibuni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ilitokea Aprili 2, 2025.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Kituo cha Afya Mugaza, Chato, kwa taratibu za uchunguzi na utambuzi.