Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Maneno Shomari (53), mkazi wa Chang'ombe jijini Dodoma, ameripotiwa kujinyonga kwa kutumia waya, chanzo kikitajwa kuwa wivu wa kimapenzi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi, tukio hilo limetokea Jumapili, Machi 30, 2025, katika Mtaa wa Site One, Area D, Kata ya Ipagala, Wilaya ya Dodoma Mjini.
Kamanda Katabazi ameeleza kuwa mwili wa marehemu ulikutwa ukining’inia kwenye moja ya miti katika eneo lake la kazi, ambapo alikuwa zamu ya kulinda usiku huo.
"Marehemu alikutwa amejinyonga kwa kutumia waya, ambao aliuning’iniza kwenye mti uliopo katika eneo lake la kazi," amesema Katabazi, akibainisha kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.