Mashambulizi ya Marekani yaua 4 Yemen, Wahouthi watishia kulipiza

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: mashambulizi-marekani-yaua-yemen-wahouthi-watishia-kulipiza-200-rickmedia

Shambulizi lililolofanywa kwa ndege ya kijeshi ya Marekani nchini Yemen limesabababisha vifo vya watu wanne huku kadhaa wakijeruhiwa.

Al Jazeera imeripoti leo Jumatano Aprili 2, 2025, kuwa watu wanne waliouawa ni waliokubwa na shambulizi lililotokea eneo la Hodeidah nchini Yemen, ikiwa ni mwendelezo wa mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya vikosi vya Wahouthi nchini humo.

Marekani pia inatajwa kupeleka meli kubwa ya pili kwa ajili ya kubeba ndege za kijeshi zitakazotumika kurusha makombora na kutekeleza mashambulizi ya kijeshi eneo la Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Waziri wa Afya wa Wahouthi, Anees Alasbahi, watu watatu wamethibitishwa kuuawa katika shambulizi la Marekani lililotekelezwa Jumanne usiku lakini idadi hiyo imeongezeka asubuhi ya leo Jumatano na kufikia watu watano.

Kundi hilo la wapiganaji wa Kihouthi lilikuwa limetishia kurejesha mashambulizi dhidi ya meli zinazohusiana na Israeli katika Bahari Nyekundu kufuatia uvunjwaji wa sitisho la mapigano huko Gaza.