Drake anazidi kuonyesha ufalme wake, aweka rekodi kwenye chati za Billboard 200

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

6 hours ago
rickmedia: drake-anazidi-kuonyesha-ufalme-wake-aweka-rekodi-kwenye-chati-billboard-200-164-rickmedia

Drake amefanikisha jambo la kihistoria baada ya albamu yake ya Nothing Was the Same kurudi kwenye chati ya Billboard 200 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2024. Hii imemfanya kuwa rapa wa kwanza kuwahi kuwa na album 10 zikiingia kwenye chati hiyo ndani wiki moja.

Album 10 zilizopatikana kwenye Billboard 200 wiki hii ni pamoja na Take Care, Views, Certified Lover Boy, For All the Dogs, Thank Me Later, Scorpion, More Life, Her Loss, $ome $exy $ongs 4 U, pamoja na Nothing Was the Same.

Hali hii inaonyesha uimara wa Drake kwenye muziki wa hip-hop na jinsi albamu zake zinavyopendwa na mashabiki wake duniani. Wengi wanasema hii ni ushahidi wa jinsi kazi yake ilivyo ya kuishi muda mrefu hata miaka mingi ikipita.