Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Rajab Abdul Kahali (Harmonize) amekanusha Taarifa za kuwa yupo kwenye Mahusiano na Mrembo Malaika Cute.
Stori za Harmonize na Malaika Cute kuwa na mahusian ya Kimapenzi zilianza muda lakini zilikuja kushika kasi zaidi baada ya Harmonize kushare video wakiwa sehemu na Malaika.
Mbali na hivyo badae alikuja kushare video ya Malaika akidai kuwa yeye sio Type yake na kuiambatanisha na Caption hii “Uki Focus na Wanao Kuchukia ni Rahisi Kuwapoteza Wanao Kupenda @malaikacute55 “
Mapema leo Staa huyo kupitia insta story yake ameshare video akiweka vitu sawa kwa kusema kuwa hakuna mahusiano ya kimapenzi kati yake na Malaika na wanaheshimiana sana.
Unaweza ukawa unajiuliza kama hawana mahusiano ya kimapenzi kweli picha zile ambazo wapo pamoja kwenye mapozi ya kimahaba walipiga kwa sababu gani?, Picha hizo zilipigwa siku wanashoot Visualizer ya Wimbo wa #Marioo #WANGU.