Mwanafunzi Wa Chuo Cha Udaktari Auawa kwa Kisu na Mpenzi Wake.

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: mwanafunzi-chuo-cha-udaktari-auawa-kwa-kisu-mpenzi-wake-455-rickmedia

Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 24 kutoka Chuo cha Mafunzo ya Udaktari cha Kenya huko Kitale aliuawa kwa kuchomwa kisu katika ugomvi unaoshukiwa kuwa wa kimapenzi nyumbani kwao.

Mwathiriwa, aliyetambulika kama #BenedictKiptoo, alikuwa mwanafunzi wa Udaktari, Majirani waliripoti kusikia fujo kutoka kwa makazi ya wapenzi hao na walipofika eneo la tukio walimkuta #Kiptoo akiwa amelala kwenye dimbwi la damu akiwa na jeraha mbaya kifuani.

Walioshuhudia walisema kuwa mpenzi huyo alitoroka eneo hilo baada ya shambulio hilo.

Moja ya sababu iliyotajwa ya Ugomvi huo #Kiptoo alichelewa kurudi nyumbani hivyo ugomvi ukatokea, Mamlaka imeanza msako wa kumtafuta mwanamke aliyehusika na shambulio hilo.