Elton John akiri kupoteza uwezo wa kuona

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: elton-john-akiri-kupoteza-uwezo-kuona-150-rickmedia

Mwanamuziki maarufu Elton John, mwenye umri wa miaka 77, amefichua kwamba amepoteza uwezo wake wa kuona vizuri baada ya kupambana na maambukizi makali. Akiwa kwenye sherehe ya hisani iliyoandaliwa kwa ajili ya shoo ya "The Devil Wears Prada: The Musical" usiku wa Jumapili, Elton alikiri kwamba hali yake ya kiafya imebadilika kwa kiasi kikubwa.

"Kamwe hatuwezi kujua hili, lakini kama baadhi yenu mtakavyokuwa mnafahamu, nilikuwa na matatizo na sasa nimeshapoteza uwezo wangu wa kuona Sijapata nafasi ya kuona shoo, lakini nimefurahi sana kusikiliza," alizungumza Elton John mbele ya wageni waliokuwa wamehudhuria sherehe hiyo kwenye Dominion Theatre, iliyopo London, sehemu ya West End.

Maelezo haya ya Elton John yaliwafanya mashabiki wake kujiuliza zaidi kuhusu hali yake ya kiafya, huku wakituma ujumbe wa pole na kumtakia uponyaji wa haraka. Aidha, msanii huyu ameendelea kuwa na mchango mkubwa katika sekta ya muziki na utamaduni duniani, licha ya changamoto anazopitia kiafya.