Staa wa Muziki kutoka Nchini Kenya, Mzaliwa wa Marekani #VictoriaKimani amefunguka sababu ambazo zimemfanya awe Single/Asiolewe mpaka leo licha ya kuwa na Miaka 39.
#VictoriaKimani amesema kuwa amekuwa Single kwa Miaka 3 na sababu kubwa iliyomfanya awe Single ni Wanaume wenyewe kwani wamekuwa ni watu wa kupenda Wanawake Wengi na kujipendelea wao tu.
Mbali na hivyo ametaja vigezo vya Mwanaume ambae anaweza kuwa nae kwenye mahusiano ambapo ni Awe Mcha Mungu, Mrefu kushinda yeye, Mwanaume ambae atamuweka wazi mbele za watu.
Mbali na hivyo amesema kuwa anaweza kuwa na mahusiano na Mwanaume ambae hana Pesa kwani anaamini wanaweza kuungana na kufanikiwa pamoja.
"Nimekuwa single kwa miaka mitatu na ni kwa sababu ya wanaume. Sababu inaweza kuwa mimi pia, naweza kuwajibika kwa kosa langu, lakini asilimia 95 ya kwanini sijaolewa ni kwa sababu ya wanaume. Siku hizi wanaume wanataka wanawake wengi"
"Ndio naweza Kuwa na Mahusiano na Mwanaume Masikini kwani naamini tukiwa pamoja tunaweza pata mafanikio"