Rapa Drake amewasilisha mashtaka dhidi ya Universal Music Group (UMG), akiwatuhumu kutumia mbinu haramu kama bots na payola ili kukuza wimbo wa Kendrick Lamar, "Not Like Us." Drake anadai UMG ilivuruga ushindani wa haki kwa kulipia umaarufu wa wimbo huo kwenye majukwaa kama Spotify na Siri.
Wakati huo huo, mtangazaji Funk Flex amefichua gharama kubwa za payola kwa DJs, akisema wasanii wanalazimika kulipa hadi dola 350,000 ili nyimbo zao zipate nafasi redioni. Flex alisema, "DJs wanapaswa kupiga muziki kutokana na ubora, si kwa malipo." Hatua hii inawafanya wasanii wachanga kushindwa kufannikiwa.
Changamoto hizi zinaibua maswali kuhusu maadili na uwazi kwenye tasnia ya muziki, huku zikiweka shinikizo kwa wadau kufanya mabadiliko yatakayosaidia wasanii chipukizi kufanikiwa.