Abdul Nondo apatikana, atelekezwa Coco Beach akiwa na majeraha

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 days ago
rickmedia: abdul-nondo-apatikana-atelekezwa-coco-beach-akiwa-majeraha-627-rickmedia

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa Chama cha ACT Wazalendo, Abdul Nondo amepatikana majira ya Saa 5 Usiku, baada ya awali kuelezwa alichukuliwa na Watu Wasiojulikana alfajiri ya Desemba 1, 2024 katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli aliposhuka kwenye basi akitokea Kigoma.

Kiongozi Mstaafu wa ACT, Zitto Kabwe, amenukuliwa na Jambo TV akisema Nondo aliokotwa na Wasamaria wema maeneo ya Coco Beach akiwa na majeraha Mwilini, akapelekwa Ofisi za ACT, kisha Hospitali ya Aga Khan kupatiwa matibabu.