Aliyekuwa RC Simiyu (Dkt.Yahaya Nawanda) ashinda kesi iliyokuwa ikimkabili

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 days ago
rickmedia: aliyekuwa-simiyu-dktyahaya-nawanda-ashinda-kesi-iliyokuwa-ikimkabili-461-rickmedia

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda ameachiwa huru baada ya kushinda kesi ya kumlawiti Mwanafunzi wa Chuo, mashtaka yaliyokuwa yakiendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza

Baada ya hukumu hiyo, Dkt. Nawanda aliyefikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 9, 2024 na kusomewa shtaka moja la kulawiti kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16. amesema “Namwachia Mungu” na akaondoka eneo la Mahakamani

Kabla ya ushahidi wa upande wa mshtakiwa kuanza kutolewa, Julai 16, 2024 mbele ya Hakimu Marley, mashahidi wawili wa Jamhuri ambao ni Mwanafunzi anayedaiwa kulawitiwa pamoja na mama mzazi wa mwanafunzi huyo walitoa ushahidi kwa utaratibu wa siri (faragha).