Mtoto wa Joe Bidden 'Hunter Bidden' aikwepa Jela, apewa msamaha wa Rais

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: mtoto-joe-bidden-hunter-bidden-aikwepa-jela-apewa-msamaha-rais-975-rickmedia

Rais Joe Biden ametoa msamaha kwa mwanaye, Hunter Biden, dhidi ya mashitaka ya makosa ya Jinai yaliyokuwa yanayomkabili, baada ya Hunter kukiri makosa hayo huku akiwa anasubiri kusomewa hukumu iliyotarajiwa kutolewa Desemba, 2024.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya White House, Biden amefanya uamuzi huo kutokana na mashtaka ya Hunter kutokuendeshwa kwa haki, tofauti na watu wengine wanaofanya uhalifu huo.