Waganga wa Zambia wakamatwa kwa jaribio la kumuua Rais Hichilema

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

11 hours ago
rickmedia: waganga-zambia-wakamatwa-kwa-jaribio-kumuua-rais-hichilema-156-rickmedia

Polisi inawashikilia Wanaume Wawili, Jasten Mabulesse Candunde na Leonard Phiri waliokamatwa Jijini Lusaka, wakituhumiwa kuwa Waganga wa Kienyeji waliokuwa na jukumu la kujaribu kumroga Rais Hakainde Hichilema.

Taarifa ya Polisi imesema Candunde na Phiri walikuwa wameajiriwa na Nelson Banda, mdogo wa Mbunge Emmanuel ‘Jay Jay’ Banda. Mbunge huyo aliripotiwa kukamatwa Novemba 2024 nchini Zimbabwe kwa tuhuma za ujambazi, madai anayoyakanusha, lakini hajaonekana hadharani tangu wakati huo.

Polisi wamesema washukiwa hao waliwaambia kuwa walikuwa wameahidiwa zaidi ya Tsh. Milioni 171 ili kufanikisha jukumu hilo, huku wakisema bado wanashikiliwa kizuizini na watafikishwa Mahakamani “hivi karibuni”.