Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni imeahirishwa usikilizaji wa Kesi ya tuhuma za Ulawiti inayomkabili Mwalimu wa Shule ya Msingi Green Acres, Saleh Ayoub hadi Januari 16, 2025 kwa maelezo kuwa Hakimu amepata udhuru.
Awali, Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa Desemba 10, 2024 Saa 4 Asubuhi lakini ikaahirishwa kutokana na Hakimu Mkazi Mkuu, Hawa Magesa kutokuwepo
Itakumbukwa mshtakiwa alipandishwa kizimbani siku moja baada ya raia kuhoji sababu za kutofikishwa Mahakamani kwa watuhumiwa aliodai walihusika na ukatili wa Mtoto husika.