Staa wa muziki kutola lebo ya WCB ,Zuchu ametangaza kumchukulia hatua kali shabiki yake anayetumia jina la Zuchu _Music katika mtandao wa kijamii wa Tik Tok.
Zuchu ambaye kwa sasa anafanya vyema kupitia wimbo wa Wale Wale ft Diamond Platnumz amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa matandao wa Instagram kwa kudai kuwa mtu huyo anatumia jina hilo vibaya kwani baadhi ya watu wanaamini ni yeye.
Msanii huyo amesisitiza kuwa yeye na Uongozi wake hauitambui akaunti hiyo pia wamesha ripoti akaunti hiyo kwenye Mamlaka husika.