Jeshi la Polisi Limewakamata Waliojaribu Kumteka Mfanyabiashara Deogratius

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 weeks ago
rickmedia: jeshi-polisi-limewakamata-waliojaribu-kumteka-mfanyabiashara-deogratius-188-rickmedia

Jeshi la polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limewakamata kundi la watu nane la wahalifu kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Songea, Ruvuma na Morogoro kufuatia tukio la utekaji la mtu aliyefahamika kwa jina la Deogratius Tarimo lililofanyika tarehe 11 Mwezi Novemba 2024 eneo la Kiluvya Wilaya ya Ubungo.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Dec 04, 2024 Jijini Dar es Salaam, Kamanda Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam CAP. Jumanne Muliro amesema pamoja na Taarifa za matukio mbalimbali, Jeshi la Polisi limekuwa likifatilia kwa ukaribu matukio hayo kwa kufanya uchunguzi wa kina, kupeleleza kwa weledi na kukusanya ushahidi

“Kundi hilo la watu nane miongoni mwao ni wa hapa Dar es Salaam, wengine wamefatwa mpaka Songea, Ruvuma na wengine eneo la Morogoro kwenye Kijiji kinachoitwa Mbingu”

Kamanda amesema watuhumiwa hao baada ya kukamatwa wamehojiwa kwa kina kuhusiana na tukio hilo lililoonyesha ushahidi kuwa ni lile la kiluvya ambalo kwa pamoja walikula njama na kila mtu kutekeleza tukio lile kaa nyakati tofauti na baadaye kufanya tukio hilo la utekaji.

Aidha Kamanda amesema katika ufuatiliaji ilibainika kwamba walitumia gari aina ya Toyota Raum ambayo wakati wakilitumia walikuwa wameweka namba za Bandia zilizosomeka namba T257EGE lakini katika ufatiliaji wake ilibainika kwamba namba ile siyo halisi bali namba halisi ni namba T237 ECF

Pia Kamanda Murilo amesema Jeshi La Polisi halivumilii na halitavumilia wala kuwa na huruma kwa mtu yoyote atakayepanga njama kufanya matukio yoyote ya kihalifu huku akitoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutoa taarifa za kweli ili jeshi kichukue hatua za kisheria kwa watu wanaopanga kufanya matukio ya kihalifu ili washughulikiwe mapema kabla ya matukio.