Wabunge 190 kati ya 300 wamepiga Kura ya kuzuia utekelezwaji wa Amri ya Rais Yoon Suk Yeol ya kutangaza Utawala wa Kijeshi, baada ya kuwatuhumu Wabunge wa upinzani kupingana na Serikali yake, pamoja na kushirikiana na Korea Kaskazini.
Muda mfupi baada ya Amri hiyo kutolewa, Vikosi vya Kijeshi viliripotiwa kuzingira Bunge kwaajili ya kutekeleza Amri ya Rais lakini Wabunge wamefanikiwa kupiga Kura na kuifuta, ambapo Spika wa Bunge, Woo Won Shik amesema Amri ya Kiijeshi ilikuwa "Batili" na kwamba Wabunge watalinda demokrasia na watu.
Kwa mujibu wa baadhi ya Sheria za Utawala wa Kijeshi ni pamoja Vyombo vya habari na machapisho yote kuwa chini ya udhibiti wa Kijeshi, Migomo na mikusanyiko inayochochea machafuko ya kijamii inapigwa marufuku, huku Watumishi wa Afya wakiwemo Madaktari waliopo kwenye Mgomo kwa zaidi ya miezi 11 wakitakiwa kurejea kazini ndani ya saa 48.