Chama Tawala cha South West Africa People’s Organisation (SWAPO) kimefanikiwa kubaki Madarakani baada ya Mgombea wake Netumbo Nandi-Ndaitwah (72), kushinda nafasi ya Urais kwa 57.31% na kuwa Rais wa kwanza Mwanamke wa Nchi hiyo.
Atakuwa Rais wa 5 wa Namibia na Mwanamke mwingine anayeingia katika orodha ya Marais Wanawake Barani Afrika, inayowajumuisha Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia (2006 - 2018), Joyce Banda wa Malawi (2012 - 2014), Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kuanzia 2021 hadi sasa, n.k
Alikuwa Makamu wa Rais wa Chama cha SWAPO chini ya Rais Hage Geingob, aliyefariki Februari 2024 na Makamu wa Rais anayemaliza muda wake, Nangolo Mbumba, aliyeendelea na jukumu la mpito baada ya kifo cha Geingob.