Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Riziki Pembe anasema licha ya Serikali kuwa na mipango mingi ya kukomesha matukio ya Ukatili na Udhalilishaji hasa kwa Wanawake na Watoto bado kuna Watu wamekuwa wakihoji kuhusu adhabu zinazotolewa kwa wanaokutwa na hatia ya makosa hayo.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Taifa ya Mtoto Ni Mboni Yangu, Desemba 14, 2024 katika Mkoa wa Mjini Magharibi amesema “Juzi kuna Mtu aliniuliza hizi adhabu zinazotolewa kwa wanaokutwa na hatia ya makosa ya ukatili na udhalilishaji, je, adhabu zake ni Miaka 30 tu basi? Nikamwambia ni Sheria zilivyosema.”
Ameongeza “Hilo suala naliacha kwa Jaji Mkuu ambapo unaweza kulifikisha kwa Wadau kisha Baraza la Wawakilishi na hatua nyingine tuone namna gani tunakwenda.”