Albamu ya Zuchu ‘Peace & Money’ kutoka Desemba 20

-rickmedia: Rick

Rick

1 week ago
rickmedia: albamu-zuchu-peace-money-kutoka-desemba-550-rickmedia

Staa wa muziki kutola lebo ya WCB ,Zuchu ametangaza kuwa ifikapo Desemba 20, 2024 ataachia rasmi albamu yake ya kwanza iitwao ‘Peace & Money’

Miongoni mwa ngoma zinazotarajiwa kutoka kwenye Albamu hiyo ni ngoma ya ‘Nimechoka’ ambayo ni ngoma ya 11 katika albamu hiyo.

Siku kadhaa zilizopita msanii huyo ametajwa kuongoza orodha ya wasanii wakike waliofanya vizuri mwaka huu.

Hii itakuwa albamu ya kwanza kwa msanii huyo tangu atambulishwe rasmi kwenye kiwanda cha muziki mwaka 2020 kupitia lebo ya WCB ambapo aliachia EP yake iitwayo 'I am Zuchu' ikiwa na ngoma zipatazo saba.