Mtanzania Ainunua Bamburi Cement Kwa Tsh.Bilioni 450

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 days ago
rickmedia: mtanzania-ainunua-bamburi-cement-kwa-tshbilioni-450-492-rickmedia

Mkurugenzi Mtendaji wa Amsons Group ( @amsonsgroup ), Mtanzania Edha Nahdi, ameongoza kufanikisha ununuzi wa asilimia 96.54 ya hisa za Bamburi Cement Plc kupitia kampuni ya Amsons Industries (K) Ltd. Ununuzi huu wa thamani ya $180 milioni sasa unamfanya Edha Nahdi na Amsons Group kumiliki rasmi Bamburi Cement, mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa saruji Afrika Mashariki.

Edha Nahdi amesema ununuzi huu unalenga kupanua uzalishaji wa saruji maalum na kuweka msingi wa ukuaji wa Amsons Group nchini Kenya, huku pia ukifungua milango kwa uwekezaji zaidi kati ya Tanzania na Kenya.

Hatua hii pia inaimarisha nafasi ya Amsons Group kama mchezaji mkuu wa kikanda Afrika Mashariki na inatoa fursa ya kushirikiana katika sekta mbalimbali za kiuchumi.