Justine Bieber aathirika kisaikolojia kuhusushwa kwenye kesi za Diddy

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 months ago
rickmedia: justine-bieber-aathirika-kisaikolojia-kuhusushwa-kwenye-kesi-diddy-204-rickmedia

Justin Bieber anadaiwa kuwa katika hali ngumu kiakili kufuatia skendo za jinai zinazomkabili rafiki yake wa zamani, Sean "Diddy" Combs.

Diddy anakabiliwa na madai ya unyanyasaji wa kingono, usafirishaji haramu wa binadamu, na madai mengine mazito.

Chanzo kimeeleza kuwa Bieber, mwenye umri wa miaka 30, amechukizwa na kila stori inayohusisha jina lake baada ya kukamatwa kwa Diddy. Justin Bieber na ameshauriwa ajiepushe kabisa na chochote kinachohusiana na Diddy.

Hata hivyo, Bieber amekuwa akilenga zaidi upande mzuri wa maisha yake, kama vile kulea mtoto wake mchanga, Jack, na mkewe Hailey Bieber.