Kanye West Kwenye Msala Mwingine Mashabiki Wataka Pesa Zao

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

17 hours ago
rickmedia: kanye-west-kwenye-msala-mwingine-mashabiki-wataka-pesa-zao-737-rickmedia

Mashabiki wa msanii maarufu wa muziki wa hip hop, #KanyeWest (YE) wamelalamikia onyesho lake la hivi karibuni mjini Shanghai na kudai warudishiwe pesa zao, wakimtuhumu msanii huyo kwa kutoa burudani isiyokuwa na viwango walivyotarajia.

Kwa mujibu wa mmoja wa mashabiki waliohudhuria tamasha hilo aliiambia #PageSix kuwa #KanyeWest alichelewa kufika jukwaani kwa zaidi ya dakika 45 na alitumia muda mwingi wa onyesho hilo kuimba kwa kutumia playback hali iliyowakasirisha wengi.

Baada ya onyesho hilo, baadhi ya mashabiki walisikika wakipaza sauti wakimtaka msanii huyo kuwarudishia fedha walizolipa kwa ajili ya tiketi, wakieleza kutoridhishwa na utendaji wake jukwaani.

Hii si mara ya kwanza kwa #YE, ambaye amekuwa akikumbwa na misukosuko mbalimbali ya kibinafsi na kijamii, kukosolewa kwa maonesho yake ya moja kwa moja. Mashabiki wengi sasa wanahoji kama bado anastahili kuheshimiwa kama msanii wa kiwango cha kimataifa.