Kerry Washngton apata nyota yake 'Hollywood Walk Of Fame'

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 weeks ago
rickmedia: kerry-washngton-apata-nyota-yake-hollywood-walk-fame-244-rickmedia

 Mwigizaji Kerry Washington (47) ameingia katika orodha ya Mastaa wa Filamu waliopata heshima ya kupewa Tuzo ya Nyota ya Hollywood Walk of Fame, kwa kutambua kazi kazi zake alizoigiza kwa takriban Miaka 30.

Washington alijizolea umaarufu zaidi akiwa ni mmoja kati ya Waigizaji wa tamthilia za Scandal, Confirmation, Little Fires Everywhere na n.k

Baada ya kupewa nyota hiyo ya heshima Kerry aliandika"Hii si nyota yangu peke yangu, ni nyota yetu,". Aliwataka mashabiki wanaotembelea Hollywood kutafuta nyota hiyo na kujivunia mchango wao katika kufanikisha ndoto yake.

Kerry Washington ameendelea kuwa msukumo mkubwa kwa wengi, akiwa mfano wa kazi ngumu, uvumilivu, na shukrani kwa safari yake ya mafanikio. Hollywood Walk Of Fame