Msanii wa muziki wa Afrobeats kutoka nchini Nigeria Ayodeji Balogun almaarufu kama Wizkid amefiwa na mama yake mzazi 'Bi Jane Dolapo Balogun' siku ya leo.
Akithibitisha tarifa ya kifo hicho kutokea Meneja wa muda mrefu wa Wizkid, 'Sunday Are' alisema Bi Balogun alifariki asubuhi ya leo Agosti 18, 2023.
Marehemu Balogun alikuwa mama wa watoto wengine wawili, Yetunde Balogun na Lade Balogun.
Mungu awe pamoja na Wizkid na familia yake kwa ujumla katika kipindi hiki kigumu.