Mapya yaibuka Juu ya kesi ya P.DIDDY, Adaiwa kutishia KISU kabla ya kubaka

-rickmedia: Rick

Rick

2 months ago
rickmedia: mapya-yaibuka-juu-kesi-pdiddy-adaiwa-kutishia-kisu-kabla-kubaka-583-rickmedia

Kadri siku zinavyozidi kwenda ndiyo Jahazi la Rapa P.Diddy linazidi kuzama. Mpaka sasa zaidi ya simu 12,000 zimepigwa na watu mbalimbali wakidai kufanyiwa ukatili wa kingono na kijinsia na Rapa huyo.

Akizungumza na Kituo cha News Nation Ariel Mitchell-Kidd  ambaye ni mwanasheria anayemsimamia mmoja wa wahanga wa Diddy amesema kuwa mteja wake amesema kuwa Diddy alimtishia kisu kabla ya kumpaka mafuta na kumbaka akishirikiana na Mlinzi wake pamoja na mwanaume mwengine ambaye jina lake halijafahamika mpaka sasa.


"Mteja wangu alibakwa na Bw. Combs, mlinzi wake, na mwanamume mwingine,” Mitchell-Kidd alisema. "Walimwalika nyumbani kwa Combs na kupanga tukio zima".