Wajumbe wa Bunge la Seneti wamezuiwa kwa muda kusafiri nje ya nchi ili kuhakikisha wote wanashiriki katika Kesi inayomuhusu Naibu Rais, Rigathi Gachagua bila usumbufu wowote. Bunge la Seneti linatarajiwa kutoa uamuzi wa shauri hilo ndani ya Siku 10 kuanzia Okt. 9, 2024.
Spika wa Seneti, Amason Kingi aliagiza Kamati zote za Bunge la Seneti ziahirishe shughuli zozote zilizopangwa kufanyika nje ya Nairobi hadi Okt.19, 2024.
Aidha, Spika Kingi amemuagiza Karani wa Seneti kumtumia barua Gachagua ya wito wa kujitetea mbele ya Seneti dhidi ya mashitaka 11 yanayomkabili kuhusu kuondolewa kwake madarakani, yakiwemo ya Matumizi mabaya ya Madaraka.