Mke wa Akon 'Tomeka Thiam' awasilisha maombi ya talaka dhidi ya Akon

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

6 hours ago
rickmedia: mke-akon-tomeka-thiam-awasilisha-maombi-talaka-dhidi-akon-721-rickmedia

Tomeka Thiam amewasilisha maombi ya talaka dhidi ya Akon, akitaja tofauti zisizoweza kupatanishwa, kwa mujibu wa nyaraka za mahakama zilizopatikana na TMZ.

Wanandoa hao, ambao wanaripotiwa kuwa wameoana tangu Septemba 15, 1996, wana mtoto mwenye umri wa miaka 17. Tomeka anataka mgawanyo wa uangalizi wa kisheria (joint legal custody) lakini akipewa uangalizi (primary physical custody) wa mtoto wao, pamoja na matunzo ya kifedha kutoka kwa Akon.

Pia ameomba mahakama ikatae kumpa Akon haki ya kupokea matunzo ya kifedha kutoka kwake.

Akon, ambaye jina lake kamili ni Aliaune Damala Badara Akon Thiam, amekuwa akiweka maisha yake ya binafsi kwa faragha, mara nyingi akizungumza kwa mafumbo kuhusu mahusiano yake.

Inasemekana anaishi maisha ya ndoa ya wake wengi (polygamy), jambo ambalo amewahi kulitaja kwenye mahojiano. Katika mahojiano na Blender mwaka 2007, Akon alisema ana watoto watano—wavulana wanne na msichana mmoja—kutoka kwa wake watatu tofauti, na kwamba ameoa mmoja wao.

Kufikia Desemba 2022, iliripotiwa kuwa tayari alikuwa na watoto tisa. Mwaka 2023, mwanamke mmoja alidai hadharani kuwa yeye ni mmoja wa wake wanne wa Akon, walioko Atlanta, Los Angeles na Afrika.

Tomeka Thiam, ambaye ametajwa kwenye maombi ya talaka, ni mmoja wa wake wachache waliotambuliwa hadharani, na ndoa yao inaripotiwa kuanza mwaka 1996.

Akon pia amehusishwa na wanawake wengine, akiwemo Rachel Ritfeld mnamo mwaka 2010, ingawa hali ya kisheria ya mahusiano haya haijawahi kufafanuliwa waziwazi.