Rapa Meek Mill ameeleza nia yake ya kutaka kupata uraia wa Ghana, akisema amechoshwa na hali ya mambo nchini Marekani.
Kupitia ukurasa wake wa X, Meek Mill ameandika, “Ninataka kupata uraia wa Ghana, kwani Marekani imejengwa kwa kubomoa wanaume weusi kama usipofuata maagizo.”
Kauli hii inakuja baada ya Meek Mill kutajwa katika orodha ya watu maarufu wanaodaiwa kuhusika katika skendo ya mapenzi na Diddy, ambaye anatuhumiwa kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.