Mahakama Kuu yaamuru Jeshi la Polisi kuwaachia wanaodaiwa kutekwa

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 days ago
rickmedia: mahakama-kuu-yaamuru-jeshi-polisi-kuwaachia-wanaodaiwa-kutekwa-299-rickmedia

Jeshi la Polisi limeagizwa kuwaachia huru au kuwafikisha Mahakamani leo Desemba 31, 2024 Watu 6 wanaodaiwa kutekwa na kushikiliwa na Polisi pamoja na Vyombo vingine vya Usalama kinyume na Sheria.

Jaji Bahati Mwamuyé ametoa amri hiyo (Habeas Corpus) inayotaka Walalamikaji hao kufikishwa Mahakamani kwa lazima leo isipokuwa tu kama Mamlaka zinazowashikilia zitatoa sababu halali ya kuzuiliwa kwao.

Matukio ya Utekaji na Watu Kupotea yameibua Maandamano ya Watetezi wa Haki za Binadamu na Wanaharakati wanaoitaka Serikali kueleza ni wapi walipo ndugu na jamaa takriban 29 ambao hawajulikani walipo hadi sasa.