Mbunge wa Kenya adai Gachagua anafadhili utekaji ili kumchafua Rais Ruto

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 days ago
rickmedia: mbunge-kenya-adai-gachagua-anafadhili-utekaji-ili-kumchafua-rais-ruto-539-rickmedia

Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni, Kimani Ichung'wah, amemtuhumu aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua kufadhili vitendo vya Utekaji na Mauaji Nchini humo kwa lengo la kuichafua Serikali ya Rais Ruto.

Ichung'wah amesema "Yule aliyekuwa Kiongozi wa Siasa za ukabila, Naibu Rais aliyepita, alikuwa akifadhili utekaji ili lawama zimwendee William Ruto. Tunawajua na tunawaona mchana na tutawatangaza mchana hadharani.”

Awali, Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya, akizungumza katika mazishi ya Mama Mzazi wa Spika wa Bunge, Moses Wetangula, alitoa wito kwa Serikali kukomesha matukio ya Utekaji, hoja inayodaiwa kuibua hisia kali kutoka kwa Wabunge wanaomteta Rais Ruto.