Kesi ya Jinai namba 34404 ya Mwaka 2024 iliyowahusisha baadhi ya Viongozi wa CCM imesomwa mbele ya Hakimu Mkazi, Rehema Mayagilo na kusimamiwa na mwendesha mashtaka upande wa Jamhuri Sauli Makori.
Imeelezwa Mahakamani hapo kuwa watuhumiwa walitenda kosa la kumuua Christina Kibiki Novemba 12, 2024 eneo Banawanu. Hata hivyo, watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwakuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea
Kibiki ambaye alikuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo, aliuawa kwa kuchomwa na vitu vyenye Ncha kali tumboni kisha kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande na kesi imeahirishwa hadi Januari 7, 2025 itakaporejea kwa ajili ya kutajwa.