Rais mpya wa Msumbiji kuapishwa Januari 15, 2025 licha ya machafuko yanayoendelea

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 days ago
rickmedia: rais-mpya-msumbiji-kuapishwa-januari-15-2025-licha-machafuko-yanayoendelea-24-rickmedia

 Baraza la Katiba (CC) limetangaza rasmi kuwa Rais Mteule, Daniel Chapo, ataapishwa Januari 15, 2025 kuwa Kiongozi wa Taifa hilo, licha ya wito wa Wananchi, Wapinzani na Jumuiya za Kimataifa kudai Uchaguzi uliompa ushindi haukuwa wa Haki, Huru na Uwazi

Ushindi wa Chapo umeibua Mgogoro na Vurugu za Kisiasa Nchini humo tangu Oktoba 2024 ambapo ripoti mbalimbali kutoka zinaeleza takriban Watu 277 wameuawa katika Maandamano ya kupinga Matokeo huku wengine zaidi ya 586 wakijeruhiwa

Aidha, Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), zaidi ya Watu 3,000 wameikimbia Nchi hiyo kutokana na machafuko yanayoendelea huku hali hiyo ikiziathiri kibiashara nchi za Malawi, Zimbabwe, Botswana na Zambia.