Angelina Jolie na Brad Pitt wakamilisha talaka yao baada ya miaka 8

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 days ago
rickmedia: angelina-jolie-brad-pitt-wakamilisha-talaka-yao-baada-miaka-819-rickmedia

Baada ya safari ndefu na yenye mvutano, Brad Pitt na Angelina Jolie hatimaye wamehitimisha talaka yao iliyodumu kwa miaka nane.

“Zaidi ya miaka nane iliyopita, Angelina aliwasilisha talaka kwa Brad Pitt. Yeye na watoto waliondoka kwenye mali zote walizoshirikiana na Brad Pitt, na tangu wakati huo amejitahidi kutafuta amani na uponyaji kwa familia yao,” alisema wakili wa Jolie, James Simon, kwenye taarifa aliyoitoa kwa Page Six.

“Hii ni sehemu moja tu ya mchakato mrefu ulioanza miaka nane iliyopita. Kusema ukweli, Angelina amechoka, lakini amefarijika kwamba sehemu hii imekamilika.”

Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza walipokuwa wakicheza pamoja kwenye filamu ya mwaka 2005, Mr. & Mrs. Smith. Wakati huo, Brad Pitt alikuwa bado amemuoa Jennifer Aniston, ambaye alitalikiana naye mwaka huohuo, huku Angelina Jolie akiwa mama wa mtoto wa kiume, Maddox, aliyemlea kutoka Cambodia tangu 2002.

Mwaka 2005, Pitt alisafiri na Jolie kwenda Ethiopia kumwasiri binti yao Zahara. Mwaka uliofuata, Pitt alihalalisha malezi ya Maddox na Zahara kabla ya kuzaliwa kwa binti yao Shiloh.