Staa #TreySongz anachunguzwa baada ya kudaiwa kumshambulia mpiga picha kwenye mgahawa huko New York.
Kwa mujibu wa TMZ, mhanga aitwaye #IsaaMansoor amesema aliajiriwa kurekodi tukio la Trey katika mgahawa wa The Ivy siku ya Jumapili asubuhi, na anadai kwamba #Trey alijua kuwa kungekuwa na kamera zinazorekodi.
Inaripotiwa kuwa hali ilizidi kuwa mbaya baada ya #Trey kukasirishwa na mashabiki waliokuwa wakimuomba kupiga naye picha. Wakati mmiliki wa mgahawa alipomuomba #Trey apige picha ya mwisho mbele ya nembo ya ukumbi huo, #Isaa anasema #Trey ghafla alimpiga ngumi kichwani, akamgonga ukutani, na kuvunja kamera zake mbili.
Mmiliki alijaribu kuingilia kati, akimwambia Trey kuwa Isaa ni mtu wake,lakini Trey anadaiwa kujibu, Sijali chochote, kisha akamsogelea mmiliki huyo kwa hasira huku amekunja ngumi.
Isaa, ambaye alikuwa ametoka hospitali siku chache kabla ya tukio hilo, anasema alipata mtikisiko wa ubongo, kichwa kuuma sana na maumivu ya kifundo cha mguu. Tayari amewasilisha ripoti polisi, na mamlaka zimethibitisha kuwa uchunguzi umeanzishwa.