Akamatwa Kwa Kumuua Mtoto wake kwa Kumchoma Kisu

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

3 months ago
rickmedia: akamatwa-kwa-kumuua-mtoto-wake-kwa-kumchoma-kisu-901-rickmedia

 Mwanaume mwenye umri wa miaka 48 amekamatwa kufatia tukio la kumchoma kisu na kumuua mwanae mwenye umri wa miaka 24 katika kijiji cha Mosobecho, Kaunti ya Nandi nchini Kenya.

Mwathiriwa alifariki dunia jioni ya Jumamosi, Agosti 31, katika Hospitali ya Rufaa ya Kapsabet nchini humo.

Kulingana na ripoti za polisi, kijana huyo aliuawa kwa kuchomwa kisu kifuani mwake katika ugomvi na baba yake ikapelekea kutokwa damu nyingi kutokana na jeraha lililotokea baada ya kuchomwa kisu.