Loading...

Baba Wa Mtoto Albino Asimwe, Paroko na Mganga Wakamatwa na Polisi Kwa Majuaji Ya Mtoto huyo

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

4 weeks ago
rickmedia: baba-mtoto-albino-asimwe-paroko-mganga-wakamatwa-polisi-kwa-majuaji-mtoto-huyo-403-rickmedia

Watu 9 wakamatwa na Jeshi la Polisi akiwemo Baba mzazi wa Mtoto #AsimweNovath , Paroko Msaidizi wakituhumiwa kuhusika na Mauji ya Mtoto huyo mwenye Ualbino aliibiwa Mei 30.2024 na mwili wake kupatikana Juni 17.2024 ukiwa umetolewa baadhi ya viungok katika kijiji cha #Makongora.

Watuhumiwa waliokamatwa ambao waliweka wazi jinsi waliovyoshiriki katika tukio hilo ni pamoja na #NovathVenant (Baba Mzazi), #ElipidiusRwegoshora (Msaidizi wa Parokia ya Bugandika) Ambae anadaiwa kumshawishi Baba wa #Asimwe wafanye tukio hilo ili wafanye biashara ya viungo vya mtoto huyo na #DesideliEvarist (Mganga wa Jadi).

Watuhumiwa wengine ni Dastan Kaiza mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman mkazi wa Nyakahama, Gozibert Alkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Rwenyagira Burkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Ramadhani Selestine mkazi wa Kamachumu na Nurduni Hamada mkazi wa Kamachumu.

Taarifa iliyotolewa Msemaji wa jeshi la Polisi DCP David Misime imeeleza kuwa Baada ya tukio hilo kutokea Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na raia wema wanaochukia vitendo vya kinyama kama hivyo walianza msako mkali kuanzia Mei 31, 2024 hadi usiku wa kuamkia Juni 19, 2024 ambapo watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na viungo vinavyodhaniwa ni vya mtoto Asimwe Novart wakiwa wamehifadhi katika vifungashio vya plastiki wakitafuta mteja.