Loading...

Mikoa 17 ina wagonjwa wa Macho Mekundu (Red Eyes) nchini Tanzania

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 months ago
rickmedia: mikoa-ina-wagonjwa-macho-mekundu-red-eyes-nchini-tanzania-735-rickmedia

Mikoa 17 imebainika kuwa na Wagonjwa wa Macho Mekundu (Red Eyes) au ‘Pink Eye Conjunctivitis’ ambapo hadi kufikia Januari 26, 2024 waliofika kwenye Vituo vya Afya walikuwa 5,359 kutoka 1,109 wa Januari 19, 2024.

Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Prof. Paschal Rugajjo, amesema “Ugonjwa umesambaa zaidi na kufikia Mikoa 17 ingawa ni Watu wachache wanafika kwenye Vituo vya Huduma za Afya.

Mikoa yenye Maambukizi hadi sasa ni Singida, Katavi, Kilimanjaro, Mara, Iringa, Njombe, Ruvuma, Simiyu, Mtwara, Lindi, Songwe, Rukwa, Mwanza, Dar, Morogoro, Dodoma na Pwani.

Kufuatia kusambaa huko, Wizara ya Afya imewaasa Wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa huo unaosababishwa na Maambukizi ya Kirusi kwenye ngozi ya juu ndani ya Jicho.