Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi amewekwa chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari baada ya kupelekwa Hospitali kutokana na kuugua maradhi ya kifua.
Taarifa ya Msemaji wa Familia, Abdullah Ali Mwinyi imeeleza kuwa kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu.
Taarifa hiyo imesema “Familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye Dua, Sala, na Maombi, tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie Shufaa ya haraka Mzee wetu pamoja na wagonjwa wengine wanaokabiliwa na maradhi mbali mbali.”