Utapiamlo na uhaba wa Chakula vyawatesa Wakimbizi Chad

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: utapiamlo-uhaba-chakula-vyawatesa-wakimbizi-chad-21-rickmedia

Idadi kubwa ya wakimbizi waliopo nchini Chad wanatajwa kusababisha uhaba wa chakula na uwapo wa utapiamlo kwa watoto nchini humo kutokana na kukosa lishe bora.

Tovuti ya African news imeripoti kuwa idadi kubwa ya wakimbizi nchini humo inasababishwa na mgogoro unaoendelea katika nchi jirani ya Sudan ambao unasababisha maelfu ya Wasudan kuvuka mpaka wao.

“Chad inahifadhi zaidi ya wakimbizi milioni moja, ikiwa ni mojawapo ya idadi kubwa ya wakimbizi barani Afrika na inayokua kwa kasi,”imesema taarifa ya ripoti hiyo.

Idadi ya wakimbizi wa Sudan nchini Chad imeongezeka maradufu katika kipindi cha miezi sita iliyopita, sambamba na jumla ya waliowasili katika kipindi cha miongo miwili iliyopita tangu mgogoro wa Darfur uanze mwaka 2003.

Chad inakabiliana na uhaba mkubwa wa chakula na utapiamlo, hasa miongoni mwa watoto, unaozidishwa na changamoto za hali ya hewa, shinikizo la kiuchumi,

kupungua shughuli za kilimo, na mivutano kati ya jumuiya.