Mke wangu amekuwa akiniroga na kunifungia Chumbani

-rickmedia: Rick

Rick

1 year ago
rickmedia: mke-wangu-amekuwa-akiniroga-kunifungia-chumbani-59-rickmedia

Mwanaume mmoja huko nchini Nigeria aliyetambulika kwa jina la Kazeem Yekini amedhamilia kumpa talaka mke wake Opeyemi kutokana na tabia ya mke wake kumnyanyasa na kumpa vitisho mbalimbali.

Bw Yekini alidai kuwa mkewe alimroga na kumsababishia hali ngumu isiyoelezeka huku akiahidi kuendelea kumchafua kwenye jamii yake. Hayo yote aliona haitoshi amekuwa akinifungia chumbani na kunizuia kufanya shughuli zangu mbalimbali.

Opeyemi alipoulizwa na mahakama alikubali tuhuma hizo na kuomba mahakama impatie haki ya kulea mtoto wao wa pekee. "Kabla ya kuja mahakamani nimejaribu kuzungumza nae ili kusuluhisha hili lakini ilishindikana. Iwapo atashikilia msimamo wake, naomba mahakama inipe haki ya kulea mtoto wa pekee kati yetu,” Opeyemi aliomba