Mahakama ya Juu imetangaza kuondoa zuio la Mtandao wa X (zamani Twitter) kwa maelezo kuwa mtandao huo umekubali kulipa faini ya takriban Tsh. Bilioni 13 (Dola Milioni 5).
Kwa mujibu wa taarifa ya Mahakama, mbali na faini Mtandao huo umekubali kumteua Kiongozi Muwakilishi ambaye ni raia wa Brazil ikiwa ni takwa la Kisheria nchini humo pamoja na kuzifunga Akaunti zilizolalamikiwa na Serikali.
Imeelezwa kuwa hatua ya kuifungia X ilisababisha Watumiaji wake takriban Milioni 22 kulazimika kutumia VPN kama njia mbadala ya kufikia huduma huku wakilalamikia Serikali juu ya uvunjwaji wa Haki ya Kupata Taarifa na Uhuru wa Kujieleza