Meta yafungia Akaunti 4,800 za Instagram na Facebook zinazoeneza taarifa za upotoshaji Nchini Marekani

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: meta-yafungia-akaunti-4800-instagram-facebook-zinazoeneza-taarifa-upotoshaji-nchini-marekani-994-rickmedia

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kampuni hiyo, imeeleza akaunti zilizofungiwa zilibainika kuwa na uhusiano na Makundi ya Ushawishi kutoka China yenye lengo la kusambaza maudhui ya chuki kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Marekani unaotarajiwa kufanyika 2024

Hatua hiyo imefanyika ikiwa ni takriban Miezi Miwili imepita tangu Idara ya Usalama wa Ndani ya Marekani ionye kuhusu Mataifa ya China na Urusi kutumia mvutano uliopo kati yake na Marekani kutengeneza maudhui yanayopotosha Wapiga Kura kupitia Akili Mnemba (AI) ili kudhoofisha Imani kwa Taasisi za Serikali na Demokrasia

Agosti 2023 Mtandao wa TikTok ulifungia akaunti 284 kutoka China zilizobainika kueneza maudhui ya chuki kuhusu masuala ya Kisiasa huku Facebook ikifuta akaunti 9,000 zilizokuwa zikiingilia mambo ya ndani ya Australia.