Jina Muhammad limekuwa chaguo kubwa kwa wazazi wanaowapa watoto wao wa kiume majina nchini Uingereza na Wales mwaka 2023, kwa zaidi ya watoto 4,600 kusajiliwa na jina hilo.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu za Kitaifa (ONS), jina hilo limekuwa miongoni mwa majina 10 maarufu tangu 2016, lakini sasa limepita jina lililokuwa likiongoza mwanzo, Noah.
Hata hivyo, kuna tofauti za kieneo, ambapo *Muhammad* halijajumuishwa kwenye majina 10 bora katika baadhi ya maeneo matatu ya England.
Matoleo mengine ya jina hilo kama Mohammed na Mohammad pia yameorodheshwa kati ya majina 100 maarufu zaidi kwa watoto wa kiume. ONS huzingatia kila tahajia kama jina tofauti, na matoleo mbalimbali ya Muhammad yamekuwa yakipendwa kwa miaka iliyopita.