Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Ibrahim Shida (24) mkazi wa Kijiji cha Sirorisimba anadaiwa kumuua aliyekuwa mke wake, Tatu Marwa (25) kwa kumchoma kisu shingoni na kumsababishia kifo.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara imesema tukio hilo limetokea Septemba 12, 2025 majira ya saa 04: 30 usiku ambapo inaelezwa kuwa baada ya kutekeleza tukio hilo mwanaume huyo aliamua kujichoma kisu hicho shingoni na kujisababishia majeraha. Hata hivyo alifariki njiani akipelekwa hospitalini.
"Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo ili kuweza kufahamu chanzo cha mauaji hayo," imeeleza taarifa ya Polisi.