Amorim amesema anakubali uamuzi wowote utakaofanywa kufuatia kichapo kingine kikali kutoka kwa wapinzani wa jiji, Manchester City, ambapo United walipigwa 3-0 kwenye derby ya Manchester matokeo ambayo yamezidi kudhoofisha rekodi yake kama kocha wa klabu hiyo.
Manchester United wamekusanya pointi nne tu katika mechi nne za msimu huu, na kufanya kuwa mwanzo wao mbaya zaidi katika kampeni ya Ligi Kuu kwa kipindi cha miaka 33.
Amorim sasa anashikilia rekodi mbaya zaidi ya ushindi (win percentage) kwa kocha yeyote wa Manchester United tangu Vita ya Pili ya Dunia.
Kwa kuongeza uzito wa hali hiyo, tangu alipoteuliwa Novemba mwaka jana, United wamekusanya pointi chache zaidi kuliko timu yoyote iliyoshiriki ligi kila msimu – wastani wa pointi moja kwa kila mechi, wakiwa na tofauti ya mabao -13.
“Tulicheza vibaya,” alisema Amorim kupitia Sky Sports. “Katika nyakati muhimu, wao walikuwa bora kuliko sisi.
“Ninajaribu kuwa na mtazamo wa kiakili. Naona rekodi. Naelewa hasira ya mashabiki na naelewa maamuzi yanayoweza kufuatwa kutokana na hali hiyo. Nakubali ukosoaji. Hilo ndilo jambo lenyewe.”
Alipoulizwa ujumbe gani anao kwa mashabiki waliokuwa wamekasirika, wengi wao wakiwemo waliotoka uwanjani kabla mechi haijaisha, Amorim alisema:
“Ujumbe wangu? Nitafanya kila kitu, kila mara nikifikiria mema ya klabu. Mpaka nitakapokuwa hapa, nitatoa juhudi zangu zote. Mengine siyo maamuzi yangu. Nateseka zaidi [kuliko mashabiki].”